Fiesta

Fiesta

Voda

Voda

Nunua

Nunua

Monday, September 19, 2016

Binti wa Donald Trump agwaya maswali mazito ya mwanahabari

Binti wa Donald Trump, mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican, Ivanka Trump
Binti wa Donald Trump, mgombea uraiswa Marekani kwa tiketi
 ya Chama cha Republican, Ivanka Trump
BINTI wa Donald Trump, mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican, Ivanka Trump, amelazimika kusitisha mahojiano na gazeti la Cosmopolitan linalochapwa baada ya kuulizwa maswali magumu.
Maswali hayo yanahusu kauli mbalimbali za baba yake huyo alizowahi kutamka kuhusu masuala ya afya ya watoto na likizo ya wazazi.
Badala ya kujibu maswali, binti huyo alimlaumu mwanahabari aliyekuwa akimhoji kwa madai kwamba maswali hayo yamegubikwa na “mambo mengi hasi”.
Binti huyo alikuwa akitaraji kuulizwa kuhusu sera mpya ya afya ya watoto ya mgombea wa Republican Donald Trump, ambayo alisaidia kuiandaa na kuitangaza rasmi wiki hii.
Mwanahabari, Prachi Gupta alimuhoji binti huyo akisema;  “Mwaka 2004 Donald Trump alisema kwamba mimba ni kitu kibaya kwa biashara. Inashangaza kuona sera hii kutoka kwake leo. Unaweza kuzungumzia matamshi hayo na labda ni kitu gani kimebadilika?”
Binti huyo hakuzubaa akajibu; “Sasa nadhani una mambo hasi sana kwenye haya maswali. Kwa mujibu wa gazeti la Cosmopolitan Ivanka akaendelea kulaumu akisema; “Kwa hiyo sifahamu ni kwa kiasi gani inasaidia kutumia muda mwingi na wewe kuhusu hili, kama unatoa matamshi kama hayo.”
Gupta aliendelea; “Ningependa kusema kwamba samahani kwa maswali – unayoyaona kwamba ni hasi. Lakini hayo maswali yana maana kwamba mgombea urais alitoa hayo matamshi wakati fulani. Kwa hiyo mimi nimekuwa nikifuatilia tu.”
Ivanka akajibu; “Ahaa, umesema kwamba alitoa hayo matamshi. Mimi sifahamu kama aliwahi kuyatoa.
Alipooneshwa chanzo cha nukuu ya baba yak ambacho ni ya Donald Trump na Shirika la Habari la NBC mwaka 2004, binti huyo akawa mkali zaidi .
Hasira za binti huyo zilikuwa dhahiri mara alipoulizwa kwa nini hoja za wakati wa kampeni kuhusu likizo haziwahusishi wenza wa mashoga au haijumuishi likizo ya kina baba ya uzazi. Lakini hata hivyo alijibu kwamba sababu ni kuwa “…nia halisi ya mpango ni kuwasaidia kina mama kupona.”
Mwandishi akauliza; “Kwa hiyo nataka kuweka hili sawa, kwa wapenzi wa jinsia moja ambao wanaokubali watoto kuwa wao, ambapo wazazi hao wawili wote ni wanaume, hawatapata likizo maalumu kwa sababu hawahitaji kupona?”
Ivanka Trump akamjibu akisema: “Hayo ni maneno yako, sio yangu. Hayo ni maneno yako. Mpango kwa sasa unaaangalia kina mama zaidi, haijalishi kama watakuwa kwenye ndoa ya jinsia moja au hapana.”
Wakati Gupta alipoanza kumuuliza ni kwa jinsi gani Donald Trump ataweza kugharimia mapendekezo yake ambayo ni ghali sana – kama vile ujenzi wa ukuta kati ya mpaka wa Marekani na Mexico, uwekezaji katika miundombinu na kuongeza matumizi ya kijeshi, Ivanka Trump alijibu kuwa mipango hiyo itagharimiwa na mpango mkuu kabambe wa mageuzi ya kodi kwa nchi hiyo.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya hapo alifanya uamuzi ‘mgumu’ wa kusitisha mahojiano hayo. “Naondoka – nalazimika kuondoka. Samahani,” alitamka.
Baadae kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ivanka Trump aliandika, “Cosmopolitan, wasomaji wenu wanajali na wanapaswa kujali kuhusu masuala yanayoawaathiri kina mama na watoto. Weka malengo panapostahili – simamia mabadiliko.”
Mtafaruku huo unajitokeza katika wakati ambao tayari timu ya kampeni ya Hillary Clinton, mgombea wa Democrat ikishutumu mpango huo wa Donald Trump kwa madai  kwamba ‘unawaangalia’ kina mama pekee na kuwasahau kina baba.
Imeandikwa na CNN na kutafsiriwa na mwandishi wa Raia Mwema

No comments:

Post a Comment